Drogba asajiliwa na Galatasaray

Image caption Didier Drogba

Galatasaray imemsajili aliyekuwa mshambulizi wa Chelsea Didier Drogba kutoka kwa klabu ya Shanghai Shenhua inayoshiriki katika ligi kuu ya Premier nchini Uchina.

Galatasaray inayocheza ligi kuu nchini Uturuki, imethibitisha kuwa Drogba amesaini mkataba wa miezoi kumi na minane na klabu hiyo.

Mchezaji hiyo mwenye umri wa miaka 34, kwa sasa yuko nchini Afrika Kusini kuiongoza kikosi cha Ivory Coast katika mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika.

Kwa mujibu wa ujumbe uliotumwa na kampuni ya uhusiano bora inayomuakilisha mchezaji huyo Sports PR Company na kuchapishwa kwa mtandano wa kijamii wa Twitter, Drogba alisema anajiandaa kurejea tena katika michuano ya kuwania kombe la klabu binga barani ulaya kwa mara nyingine.

Galatasaray imefuzu kwa raundi ya muondoana ya kuwania kombe hilo na imepangiwa kucheza na FC Schalke 04 kutoka uUjerumani.

''Hii ni fursa nzuri ya kuichezea timu kubwa na ni nafasi ambayo siwezi kupuuza'' Alisema Drogba.

Shenhua yapata pigo

Image caption Wesley sneijder

Agenti wam mchezaji huyo amesema, Drogba atajiunga la klabu hiyo ya Galatasaray baada ya kukamilika kwa michuano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika.

Drogba ni mchezaji wa pili wa hadhi ya juu kusajiliwa na Galatasaray baada ya Wesley Sneijder aliyejiunga na klabu hiyo kutoka klabu ya Inter Milan.

Drogba alijiunga na Shanghai Shenhua mwezi juna mwaka uliopita na ameifunga jumla ya magoli manane baada ya kucheza mechi kumi na moja.

Awali Drogba alitaka kurejea Ulaya kwa mkopo na klabu yake ya zamani ilikuwa imeanzisha mazungumzo ya kumsajili.

Lakini shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA lilipinga uhamisho huo, likisema kuwa linakiuka sheria za kimataifa kuhusu uhamisho na usajili wa wachezaji.

Mchezaji mwingine wa zamani wa Cheslea Nicolas Anelka huenda pia anajiandaa kukihama klabu hiyo ya Shenhua, baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu katika klabu ya Juventus.