Je Chipolopol itazima mikiki ya Burkina Faso?

Image caption Mabingwa watetezi wa kombe la mataifa ya Afrika

Mabingwa watetezi wa kombe la mataifa bingwa barani Afrika, Chipolopolo ya Zambia, leo ni sharti iilaze Burkina Faso, katika mechi yao ya mwisho ya Kundi C , ili ifuzu kwa robo faniali.

Ikiwa Zambia itapoteza mechi hiyo iytakuwa imeandikisha rekodi ya kuwa bingwa wa kwanza mtetezi kuwahi kushikilia kombe hilo kwa muda mfupi zaidi ya kuondolewa kwenye hatua ya makundi.

Image caption Wachezaji wa Burkina Faso

Burkina Faso nayo inahitaji kutoka sare ya aina yoyote na Zambia ili ijikatie tikiti ya robo fainali hizo.

Hata hivyo, Burkina Faso inakabiliw ana wakati mgumu kwa kuwa itakosa huduma za kipa wake wa kwanza Abdoulaye Soulama, ambaye anakamilisha adhabu yake ya kutocheza mechi mbili, baada ya kupewa kadi nyekundu.

Mcheza kiungo matata wa Burkina Faso Alain Traore anatarajiwa kukiongoza kikosi hicho kufuzu kwa robo fainali hizo.

Traore amefunga magoli matatu zikiwemo mbili wakati wa mechi yao dhidi ya Ethiopia ambayo walishinda kwa magoli manne ya yai.

Zambia haijawahi kushindwa na Burkina Faso katika michuano ya kuwania kombe la mataifa bingwa barani Afrika.

Algeria, ndio mabingwa watetezi wa mwisho kuwahi kuondolewa katika raundi ya kwanza, baada ya kushinda kombe hilo mwaka wa 1990.