Togo 1 Tunisia 1

Image caption Wachezaji wa Tunisia

Mechi ya mwisho ya makundi kati ya Togo na Tunisia, moja ya mechi ngumu zaidi katika fainali za mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu inaendelea.

Hii ni kutokana na kuwa timu hizo mbili zina alama mbili kila mmoja naTogo inahitaji ushindi ili kufuzu kwa hatua ya robo fainali nayo Tunisia ikihitaji sare ya aina yote ili isonge kwa hatua ijayo.

Togo ilianza mechi hiyo kwa vishindo huku ikipata bao lake la kwanza kunako dakika ya 12 kupitia kwa mchezaji Serge Gakpe ambaye alipokea pasi nzuri kutoka kwa nahodha wa timu hiyoEmmanuel Adebayor.

Emmanuel Adebayor ndiye anayetarajiwa kuongoza kikosi cha Togo katika harakati zao za kufuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo kwa mara ya kwanza.

Kunako dakika ya 30 Tunisia ilizawazisha kupitia mkwaju wa penalti baada ya mshambuliaji wake Walid Hichri kuangusha kwenye eneo la hatari na Dare Nibombe.

Togo itajilaumu kwa kukosa kutumia nafasi iliyopata wakati wa mechi hiyo.

Emmanuel Adebayor alipoteza nafasi nzuri sana dakika za mwanzo mwanzo za mechi hiyo na kadri mechi inavyoendelea, ndivyo wachezaji wa Tunisia wanvyoendelea kuimarika.

Khaled Mouelhi ndiye aliye tunukiwa jukumu hilo la kuupiga mkwaju huo na bila ya kusita akaupachika wavuni, na kwa mara nyingine kufufua matumaini ya Tunisia ya kufuzu kwa robo fainali.

Baada ya dakika za kwanza 45, timu hizo mbili zilitoshana nguvu.

Tunisia ilianza kipindi cha pili huku ikiwa na nguvu zaidi na nusura ifunge bao la pili lakini mshambuliaji wake Oussama Darragi aliangushwa na Vincent Bossou.

Wachezaji wa Tunisia walimtaka refa wa mechi hiyo kuwapa penalti lakini ombo lao lilikataliwa baada ya muamuzi huyo kuamua hawakustahili.

Kocha wa Tunisia Sabi Trabelsi alifanya mabadiliko kadhaa ili kuongeza nguvu kikosi chake.

Kocha huyo alimuondoa mshambuliaji wake mmoja Wahbi Khazri na mahala pake kuchukuliwa na Zouheir Dhaouadi ambaye anaweza kuchezakucheza safu ya kati na ushambuliaji.

Dakika ya sabini na nane, Tunisia ilipoteza nafasi nzuri ya kufunga bao la pili, pale mchezaji wake alipopoteza kwaju wa penalti.

Wachezaji kadhaa wa Togo walipinga uamuzi huo wa refa hatua iliyopelea wawili wao kupewa kadi ya njano.

Togo haijawahi kufuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo.