Togo 1 Tunisia 0

Image caption Wachezaji wa Tunisia

Mechi ya mwisho ya makundi kati ya Togo na Tunisia, inakisiwa kuwa moja ya mechi ngumu zaidi katika fainali za mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu.

Hii ni kutokana na kuwa timu hizo mbili zina alama mbili kila mmoja naTogo inahitaji ushindi ili kufuzu kwa hatua ya robo fainali nayo Tunisia ikihitaji sare ya aina yote ili isonge kwa hatua ijayo.

Togo ilianza mechi hiyo kwa vishindo huku ikipata bao lake la kwanza kunako dakika ya 12 kupitia kwa mchezaji Serge Gakpe ambaye alipokea pasi nzuri kutoka kwa nahodha wa timu hiyo Emmanuel Adebayor.

Emmanuel Adebayor ndiye anayetarajiwa kuongoza kikosi cha Togo katika harakati zao za kufuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo kwa mara ya kwanza.

Tangu miaka minane iliyopita, Adebayor amekuwa mmoja wachezaji muhimu zaidi katika kikosi cha Togo, lakini uhusiano wake wa maafisa wa shirikisho la mchezo wa soka nchini Togo, haujakuwa wa kuridhisha.

Togo haijawahi kufuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo, na ikiwa itafanikiwa katika mechi ya leo basi itakuwa imeandikisha historia.