Afrika Kusini 1 Mali 1

Image caption Wachezaji wa Afrika Kusini

Mali tayari imesawazisha goli dhidi ya Afrika Kusini na sasa matokeo ni 1-1.

Goli la Afrika Kusini limefungwa katika dakika ya 31 na Tokelo Rantie.

Afrika Kusini inapigana kushinda pambano hili ili kutimiza ndoto yake ya kutwaa kombe hilo kama ilivyofanya mwaka 1996 ilipoandaa mashindano hayo.

Afrika Kusini ilifuzu kucheza robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ikiwa mshindi wa kwanza kutoka kundi A, huku Mali wakitokea kundi B wakiwa washindi wa pili.

Image caption Kikosi cha Mali

Mchezo umekuwa ni wa kushambuliana, Afrika Kusini ikinufaika zaidi na umati mkubwa wa washangiliaji.

Hata hivyo Mali imesawazisha goli hilo katika dakika ya 58 kipindi cha pili likifungwa na Seydou Keita.