Ghana 1 Burkina Faso 0

Image caption Timu ya Ghana

Sasa ni kipindi cha pili Ghana ikiwa bado inaongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Burkina Faso, ukiwa ni mchezo wa pili wa nusu fainali za kombe la mataifa ya Afrika.

Goli la Ghana limefungwa na Mubarak Wakaso kwa njia ya penalti katika dakika ya 13, baada ya mshambuliaji wa Ghana Atsu kuangushwa katika eneo la hatari.

Kikosi cha kocha Kwesi Appiah kina wachezaji wa kimataifa na wale wanaocheza ligi ya nyumbani. Kifuatacho ni kikosi cha Black Star na timu wanazochezea katika mabano.

Walinda mlango: Adam Larsen Kwarasey (Stromgodset, Norway), Fatau Dauda (AshantiGold), Daniel Agyei (Liberty Professionals)

Walinzi: John Paintsil (Hapoel Tel Aviv, Israel), Harrison Afful (Esperance, Tunisai) Richard Kissi Boateng (Berekum Chelsea), Mubarak Wakaso (Espanyol, Spain), John Boye (Stade Rennes, France), Isaac Vorsah (Salzburg, Austria), Rashid Sumaila (Asante Kotoko), Jonathan Mensah (Evian, France), Jerry Akaminko (Eski┼čehirspor, Turkey), Mohammed Awal (Maritzburg United, South Africa)

Wachezaji wa Kati: Emmanuel Agyemang Badu (Udinese, Italy), Anthony Annan (Osasuna, Spain), Rabiu Mohamed (Evian, France), Derek Boateng (Dnipro, Ukraine), Kwadwo Asamoah (Juventus, Italy), Solomon Asante (Berekum Chelsea), Albert Adomah (Bristol City, England), Christian Atsu (Porto, Portugal), Andre Ayew (Olympique Marseille, France)

Washambuliaji: Asamoah Gyan (Al Ain, United Arab Emirates), Richmond Boakye Yiadom (Sassuolo, Italy), Emmanuel Clottey (Esperance, Tunisia), Yahaya Mohamed (Amidaus Professionals).

Image caption Kikosi cha Burkina Faso

Kwa upande wa Burkina Faso timu yenye kuonyesha mchezo mzuri na wa ushindani katika fainali hizo, pia ina wachezaji wa Kimataifa na wale wanaocheza ligi ya nyumbani.Moumouni Dagano nahodha wa timu ya Burkina Faso amewahimiza wenzake kupigana kufa kupona ili waweze kucheza fainali.

Kikosi cha Burkina Faso kinatarajiwa kuwa na wachezaji wafuatao:Soulama Abdoulaye, Ahmed Da-Hugues,Bakary Kone,Koffi Mohamed, Djakaridja Kone, Florent Rouamba, Keba Paul, Moumouni Dagano(nahodha), Jonathan Pitriopa, Mady Panandatiguiri na Aristide Bance.