Bingwa 2013, Nigeria au Burkina Faso?

Image caption Burkina Faso

Mbabe wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013, atajulikana Jumapili baada ya miamba ya soka barani Afrika, Nigeria na Burkina Faso kupambana katika mchezo wa fainali.

Fainali za mwaka huu zinazofanyika nchini Afrika Kusini, zilishirikisha timu 16, huku mabingwa watetezi wa kombe hilo, Zambia, waking'olewa katika hatua ya makundi.

Timu nane zilisonga hatua ya robo fainali. Timu hizo ni Afrika Kusini, Burkina Faso, Cape Verde, Ghana, Ivory Coast, Mali, Nigeria na Togo.

Nigeria ambayo ilianza kwa kusuasua katika hatua ya makundi, imeonyesha mchezo mzuri katika mechi zake zilizofuata kuanzia ngazi ya robo na nusu fainali.

Ikicheza hatua ya robo fainali, Nigeria iliifunga Ivory Coast mabao 2-1, huku Ghana ikiifunga Cape Verde mabao 2-0.

Baada ya kutinga nusu fainali, Nigeria iliiadhibu Mali magoli 4-1. Nayo Burkina Faso ikishinda magoli 3-2 kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya 1-1 dakika 120 za mchezo.

Mali sasa itapambana na Burkina Faso kutafuta mshindi wa tatu siku ya Jumamosi.

Iwe isiwe, bingwa ni kati ya Nigeria na Ghana.