Fulham yaibwaga Stoke City 1-0

Image caption Barbatov mshambuliaji wa Fulham

Dimitar Berbatov alifunga bao moja na kuongoza klabu yake ya Fulham kuilaza Stoke City kwa bao moja kwa bila katika mechi ya kusisimua ya ligi kuu ya premier nchini England.

Ushindi wa leo ni wa nne kwa klabu hiyo katika mechi kumi na tisa zilizopita za ligi kuu ya premier.

Berbatov alivurumisha kombora kali kutoka umbali karibu mita muda mfupi kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza.

Image caption Jonathan Walters mshambuliaji wa Stoke City

Katika kipindi cha pili timu hizo mbili zilionekana kutoshana nguvu huku kila moja ikifanya mashambulio katika lango la mwenzie.

Stoke ilipoteza nafasi nzuri ya kusawazisha dakika za mwanzo za kipindi cha pili wakati mkwaju wa penalti uliopigwa na Jonathan Walters kudakwa na kipa wa Fulham Mark Schwarzer.

Kufuatia ushindi huo Fulhan sasa ina pointi tisa mbele ya timu inayoshikilia nafasi ya kumi na nane na hivyo kujiondolea fedheha ya kushushwa daraja msimu ujao.