Barcelona yakaangwa na Real Madrid

Image caption Wachezaji wa Real Madrid wakisherehekea bao lao

Real Madrid imedhihirisha kuwa bado ingali mbabe wa soka nchini Uhispania baada ya kuilaza Barcelona kwa magoli matatu kwa moja katika mechi kali ya marudiano ya kuwania kombe la Copa del Rey siku ya Jumanne usiku katika uwanja wa Nou Camp.

Cristiano Ronaldo aliifungia Real Madrid bao lao la kwanza kupitia mkwaju wa penalti baada ya kuangushwa kwenye eneo la hatari na mlinda lango wa Barcelona Gerard Pique.

Juhudi za nyota wa Barcelona Lionel Messi kusawazisha ziliambulia patupu pale mikwaju yake ikidakwa na kipa wa Real Madrid.

Ronaldo aliizidhishia Barca masaibu pale alipofunga bao la pili baada ya kupata pasi kutoka kwa Angel di Maria.

Matatizo ya Barcelona hayakuishia hapo na mshambulizi wa real Raphael Varane alifunga bao la tatu kwa kichwa na hivyo kuhakikisha kuwa Real inasonga mbele ya mashindano hayo.

Kufikia sasa Real imo alama 16 nyuma ya Barcelona katika msururu wa ligi kuu ya la liga na wiki ijayo imepangiwa kuchuana na Manchester United katika mechi ya marudiano ya kuwania kombe la klabu bingwa barani ulaya.

Real sasa imejikatia tikiti ya fainali ya mashindano hayo ya Copa del Rey na itacheza dhidi yuan mshindi wa mechi kati ya Sevilla na Atletico Madrid.

Kati ya mechi kumi kati ta timu hizo mbili, Barcelona ilikuwa imeshunda mechi tano na katika mechi ya hiyo, Real Madrid ilitawaka kwa kiasi kikubwa.