Giggs asaini mkataba mpya

Ryan Giggs

Ryan Giggs, amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja na klabu ya Manchester United.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39, sasa atasalia na Manchester United, hadi juni mwaka wa 2014, na kukamilisha msimu wake wa 23 kama mmoja wa wachezaji kumi na mmoja wa kwanza wa Manchester United.

Nahodha huyo wa zamani wa Scotland, alicheza mechi yake ya kwanza na Manchester United tarehe mbili mwezi machi mwaka wa 1991 na maefunga magoli 168 baada ya kucheza mechi 931.

''Nahisi vyema, na ninafurahia kucheza hata zaidi na jambo muhimu zaidi ni kuwa ninachangia pakubwa katika ufanisi wa klabu yangu'' Alisema Giggs.

Giggs, amesema, ni fahari yake kuwa katika moja ya vilabu kubwa zaidi duniani na kuwa kwa sasa wana hamu ya kushinda zaidi huku msimu ukikaribia kumalizika.

Kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amesema, Ryan ni mfano mzuri, jinsi alivyo na jinsi anavyojitunza.

Kwa mujibu wa kandarasi hiyo mpya Giggs sasa atacheza hata baada ya kuhitimu umri wa miaka 40 tarehe 29 mwezi Novemba mwaka huu.

Giggs amewahi kushinda mataji kumi na mbili ya ligi kuu, nne za kombe la FA na matatu ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya.

Alicheza mechi sitini na nne na timu ya Taifa ya Scotland kabla ya kustaafu mwaka wa 2007 na pia aliongoza kikosi cha timu ya taifa ya soka ya Uingereza katika michezo ya olimpiki mjini London.