Anichebe kutaichezea Nigeria kwa muda

Victor Anichebe
Image caption Victor Anichebe mshambulizi wa Everton

Shambulizi wa Everton Victor Anichebe ametangaza kuwa amestaafu kwa muda kama mchezaji wa timu ya taifa ya Nigeria,Super Eagles ili kuchunguza na kuipa mwili wake nafasi ya kupona vyema.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, aliyezaliwa mjini Lagos, ameiambia BBC kuwa kwa sasa hataki kujumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria.

Anichebe alikuwa miongoni mwa wachezaji waliotarajiwa kujumuishwa kwenye kikosi cha Nigeria kitakacho shiriki la michuano ya kufuzu kwa kombe la dunia na kombe la shirikisho mwezi Juni mwaka huu.

Katika miezi ya hivi karibuni, mchezaji huyo amekuwa na majeraha kadhaa ikiwemo lile la paja ambalo alilipata wakati wa mechi kati ya Nigeria na Madagascar mwaka wa 2011.

Hata hivyo amesema licha ya kuwa ni fahari yake kuichezea taifa lake, nia yake kuu kwa sasa ni kujitolea ilio kuhakikisha kuwa klabu yake ya Everton inasalia kwenye ligi kuu ya Premier msimu ujao.

Mchezaji huyo wa zamani ya timu ya vijana chipukizi ya Uingereza alibadilisha uaraia wake mwaka wa 2008, na kuichezea timu ya Nigeria kwa mara ya kwanza mwaka wa 2008.

Alifunga katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Afrika Kusini, bao ambalo liliisaidia Nigeria kufuzu kwa michezo ya Olimpiki mwaka wa 2008 na alikuwa katika kikosi kilichoshinda medali ya fedha mjini Beijing.