Sessegnon apigwa marufu mecchi tatu

Image caption Wachezaji wa Sunderland wakicheza na Aston Villa

Mshambulizi wa Sunderland Stephane Sessegnon, sasa atakosa mechi zote za ligi kuu ya Premier zilizosalia, baada ya jopo huru la shirikisho la mchezo wa soka nchini England, kufutilia mbali rufaa yake.

Sessegnon, alikuwa amekata rufaa kupinga kadi nyekundu aliyopewa wakati wa mechi yao na Aston Villa Jumatatu Usiku.

Refa wa mechi hiyo Lee Probert, alimpaa Sessegnon, kadi nyekundu moja kwa moja baada ya kumfanyia madhambi Yacouba Sylla katika kipindi cha pili cha mechi hiyo ambayo Aston Villa ilishinda kwa magoli sita kwa moja.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, hatashiriki katika mechi za Sunderland zilizosalia msimu huu, dhidi ya Stoke City,Southampton na Tottenham, huku kocha wa klabu hiyo Paolo Di Canio, akiendelea juhudi za kuinusuru klabu hiyo kutokana na tishio la kushushwa daraja msimu ujao.