Villas-Boas: lazima Gareth Bale abaki

Image caption Gareth Bale mshambulizi wa Tottenham

Andre Villas-Boas amesema ikiwa klabu ya Tottenham inataka kufanya vyema msimu ujao basi lazima wamuhifadhi mchezaji Gareth Bale.

Spurs iliteleza kuingia katika michuano ya Klabu Bingwa bara Ulaya katika michuano ya siku ya mwisho wa Ligi kuu ya Uingereza baada ya Arsenal kuwafunga Newcastle 1-0 hivyo kumaliza ligi wakiwa alama moja juu ya Tottenham.

Kuna hofu kuwa mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 23 huenda akahama kutokana na Spurs kushindwa kufunzi katika mashindano hayo ya bara Ulaya.

Lakini Villas-Boas amesema: "ikiwa tunataka kufaunye vizuri zaidi msimu ujao nilazima tushikilie hazina yetu na hilo ndilo nimekuwa nikifahamishwa tangu awali".

Bale, ambaye anadaiwa kunyemelewa na timu kadhaa maarufu miongoni mwao Real Madrid aliifungua Spurs bao lao la ushindi dhidi ya Sunderland siku ya mwisho wa Ligi kuu ya Uingereza.

Licha ya ushindi huo bado Spurs ilimaliza katika nafasi ya tano, ikiuwa nyuma ya Arsenal.

Villas-Boas amesisitiza kuwa msimu ujao timu yake itafufuka na kuwa katika nafasi bora zaidi ya kufuzu katika michuano ya Klabu bingwa bara ulaya.