Real Madrid yamtaka Carlo Ancelotti

Image caption Carlo Ancelloti kocha mwenye sifa kem kem

Wakati Real Madrid ikitangaza kuwa inamtaka Kocha Carlo Ancelotti timu yake ya Paris St-Germain ya Ufaransa imsema haiwezekani yeye kuhama.

Wiki iliyopita maombi ya klabu hicho cha Uhispania yalikataliwa na mabingwa hao wapya wa Ufaransa.

Sasa Ancelotti mwenyewe ametangaza kuwa anataka kuondoa Ufaransa na kuijunga na Real Madrid

"nimewaomba kuondoka na hadi sasa bado nasubiri jubu lao," Ancelotti, wenye umri wa miaka 53 amesema.

Lakini Rais wa PSG Nasser al-Khelaifi mwenye makao yake Qatari amesema: " ameomba kuondoka na kujiunga na Real Madrid , hii haiwezekani kwa sababu kwa muujibu wakandarasi yake bado amesalia na mwaka mmoja, kwa hiyo huo ndio uamuzi wetu".

Akizungumza na kituo kimoja cha Televisheni cha Qatari rais huyo amesema : " hiyo ni shauri yake; sio tatizo letu . Mbali na mwaka mmoja uliosalia tumetangaza kumuongezea mwaka mmoja zaidi . Ukiwa na mkataba unapaswa kuuheshimu".

Hadi sasa Jose Mourinho ni Meneja wa Real Madrid inagawa imetangazwa kwamba anarudi Chelsea msimu ujao.