Serena Williams aibuka mshindi Ufaransa

Image caption Serena Williams

Mchezaji anayeorodheshwa nambari moja duniani kwa kina dada Serena, ameshinda kombe lake la pili la mashindano ya Tenis ya French Open, miaka kumi na moja baada ya kushinda tuzo hilo kwa mara ya kwanza.

Serena Williams alimshinda bingwa mtetezi wa mashindano hayo Maria Sharapova wa Urussi kwa seti mbili kwa moja za 6-4,6-4.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka thelathini na moja kutoka Marekani alitumia muda wa saa moja dakika arubaini na sita kumpiku mpinzani wake.

Ushindi huo ni wa kumi na sita kwa mchezaji huyo katika mashindano ya tennis ya Grand Slam na anakaribia kusawazisha rekodi iliyowekwa na Martina Navratilova na Chris Evert ambao wamashinda mataji kumi na nane kila mmoja.

Serena ambaye hajashindwa katika mashindano thelathini na moja yaliyopita, wengi wanahisi kuwa ana nafasi nzuri sana ya kushinda taji lingine mwezi ujao wakati wa mashindano ya Wimbledon.

Kabla ya ya fainalio hiyo Sharapova, alikuwa amehaidi kuwa atafanya kila juhudi kumshinda mchezaji huyo kutoka Marekani baada ya juhudi zake za kumuangusha katika mashindano kumi na mawili yaliyopita kutumbukia nyongo.