Uganda yafufua safari ya Brazil

Image caption Wachezaji wa Uganda

Timu ya Taifa ya Soka ya Uganda, leo imeilaza Liberia kwa bao moja kwa bila na kuimarisha matumaini yake ya kufuzu kwa kombe la dunia mwaka ujao nchini Brazil, katika mechi kali iliyochezwa mjini Kampala.

Kufuatia ushindi huo Uganda Cranes sasa imepanda hadi nafasi ya pili katika kundi J na alama 5 nyuma ya vinara wa kundi hilo Senegal ambao wanachuana na Angola.

Uganda sasa imesalia na mechi mechi mbili na imepangiwa kuchuana na Angola tarehe kumi na tano mwezi huu kabla ya kupepetana na Senegal tarehe 6 Septemba mwaka huu katika uwanja wa Leopold Senghor.

Uganda ni sharti ishindi mechi zake zilizosalia ili kuwa katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa fainali hizo zitakazoandaliwa nchini Brazil Januari mwakani.

Katika mechi zingine za kufuzu kwa Fainali hizo, Zambia wameilaza Lesotho kwa magoli manne mwa yai nayo Botswana wakalemewe nyumbani kwao na Ethiopia kwa kufungwa magoli mawili kwa moja.