Gor Mahia yatoka sare na City Stars

Neymar aumwa
Image caption Neymar aumwa

Gor Mahia leo hii imetoka suluhu na City Stars huku Tusker ikishinda Chemilil Sugar bao 1-0 magharibi mwa Kenya kati ya mechi kadhaa za ligi kuu ya Kenya zilizochezwa leo.

Licha ya sare hiyo,Gor Mahia bado inaongoza ikiwa na pointi 37 ikifuatiwa na Thika United na AFC Leopards.

Leopards jana imeinyoa Ulinzi bao 1-0, mfungaji akiwa ni Allan Wanga alipounganisha krosi ya Charles Okwemba.

Muhoroni Youth ilishinda Sofapaka 1-0 na KCB ikaongeza machungu kwa Homeboyz ya magharibi mwa Kenya ilipoizaba mabao 2-1..

Katika habari za Kimataifa ingawa ni barani Afrika, Mbwana Samata amefululiza na mwendo mdundo wa kufunga katika kila mechi akiongoza na kuiweka kifua mbele Klabu yake ya TP Mazembe katika michuano ya Kombe la Shirikisho kwa kuinyuka FUS Rabat ya Morocco bao 3-0.

Hadi mechi hio Mbwana mwenye umri wa miaka 21 kutoka Tanzania amefunga mara nne katika mechi nne ambapo Mazembe ikitafuta ufanisi.

Itakumbukwa kua Mbwana Samata amefunga katika mechi zote za nyumbani na ugenini dhidi ya Liga Muculmana ya Msumbiji kisha katika mchuano mwingine wa ufunguzi dhidi ya Entente Setif ya Algeria majuma mawili yaliyopita.

Ushindi wa Mazembe katika mji wa Lubumbashi dhidi ya washindi wa Kombe la shirikisho mwaka 2010 unaiweka Mazembe kwenye kilele cha Kundi B.

CA Bizertin ya Tunisia ilitizamiwa kupambana na Setif baadaye jumapili kwa mchuano mwingine wa kundi hili la B ingawa uwanja ulipanga kua chini ya ulinzi mkali kutokana na hali ya mbovu ya kisiasa inayopitia Mataifa ya Kiarabu.

Washindi wa kombe hili mnamo mwaka 2006 waliiondoa klabu ya St Geaoge kutoka Ethiopia 2-1 mjini Sousse.

Ushindi huo ulikua mgumu baada ya Mohamed Nafkha kujifunga bao mwenyewe lakini Issam Jbali alirudisha bao hilo kabla ya Baghdad Bounedjah kupata la ushindi katika kipindi cha pili.

Na hapa Ulaya Klabu ya Barcelona imetangaza kua mchezaji wao mgeni kutoka Brazil Neymar amepatikana kua na upungufu wa damu mwilini, ingawa hilo halitomzuia kuendelea na mazowezi.

Klabu hiyo imeongezea kusema kua Neymar alikumbwa na tatizo hilo la upungufu wa damu kufuatia operesheni ya findo au tonsilitis.

Maradhi haya ni kupungua kwa kipimo cha seli nyekundu za damu ambazo husababishia mgonjwa kujihisi mchovu au dhaifu mara kwa mara.