Ni Messi, Ronaldo au Ribery tuzo ya UEFA

Image caption Ronaldo na Messi kwenye tuzo zilizopita

Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Franck Ribery watachuana kuwania tuzo ya shirikisho la kandanda barani ulaya UEFA kuwa mchezaji bora wa Ulaya katika msimu uliopita..

UEFA ilitangaza majina ya wanasoka hao watatu siku ya Jumaanne baada ya awali kutangaza orodha ya wachezaji kumi bora walioteuliwa na waandishi habari wa nchi wanachama za UEFA..

Ribery ni miongoni mwa wachezaji wanne wa klabu bingwa ya Ulaya Bayern Munich wanaotoa changamoto kwa wachezaji wawili mashuhuri wanaosifiwa katika kandanda ya barani Ulaya.

Tuzo hiyo itatolewa Agosti 29 mwaka huu 2012 wakati wa droo ya michuano ya klabu bingwa ya Ulaya mjini Monaco baada ya kupigiwa kura na jopo la wanahabari..

Messi alishinda tuzo ya kwanza misimu miwili iliyopita na mwenzake wa klabu ya Barcelona, Andres Iniesta alishinda mwaka jana.