Drogba wafunzwa soka na Mexico

Timu ya Ivory Coast siku ya Jumatano usiku ilionyeshwa kivumbi kwa kuchunwa mabao 4-1 na Mexico katika mechi ya kirafiki New Jersey , Marekani

Image caption Mechi kati ya Ivory Coast na Mexico

Mexico ambao walifika katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la CONCACAF walipata mabao yao matatu katika kipindi cha kwanza.

Washambuliaji wa Mexico walipata mabao yao mawili kufuatia safi ya ulinzi ya Ivory coast kufanya makosa.

Mlinzi Arthur Boka aliwazawadi Mexico bao la kwanza alipojifunga kabla ya mshambulizi Oribe Peralta kuifungia Mexico mabao mawili.

Na katika dakika ya 60 mwamba Didier Drogba aliipatia Ivory Coast bao la kufutia machozi.

Firimbi ya mwisho Mexico nne, Ivory Coast bao Moja.