Uingereza yailima Scotland kibahati

Image caption Mechi ya Kirafiki kati ya Uingereza na Scotland

Kijana Rickie Lambert aliookoa jahazi la Uingereza pale alipofunga bao la ushindi mara tu alipoingia uwanjani katika mpambano uliogaragazwa katika Uwanja wa Wembley.

Hii ni mechi ya kwanza kabisa kwa Lambert kuichezea Uingereza.

Awali mchezaji James Morrison aliipatia Scotland bao la mapema baada ya kuchomoa shuti kali lililomshinda mlinda lango wa Uingereza Joe Hart kuzuia

lakini baadae msambulizi Theo Walcott alisawazisha bao hilo baada mchezo safi .

Hata hivyo furaha ya Uingereza haikudumu kwani dakika chache baadae Kenny Miller aliiweka Scotland kifua mbele kwa mkwaju mkali ambao kipa wa Uingereza hakuoona.

Baada ya kipyenga cha mwisho mashabiki wapatao 80,000 waliinuka vitini mwa wakiwa wameridhika na jinsi maasimu hao wawili wa soka walivyosakata kabumbu.