Mourinho aiwazia mechi ya kwanza

Image caption Jose Mourinho kocha wa Chelsea

Kocha wa Chelsea,Jose Mourinho amesema itakua vigumu kujizuia wakati atakapokaa rasmi katika benchi ya Stamford Bridge kwa pambano lao la kwanza la Ligi Kuu ya Premier dhidi ya Hull City.

Mourinho aliyejunga tena na klabu hiyo kwa awamu ya pili mnamo mwezi wa Juni baada ya kuondoka mwaka September 2007.

"Nitakapoingia katika uwanja wangu,kukaa katika benchi langu pamoja na watu wangu ,itabidi niwe mtulivu kidogo,"Alisema Mourinho,mwenye umri wa miaka 50.

"Itanichukua dakika mbili tatu kutafakari na kabla ya kushughulikia pambano lenyewe ."

Mourinho aliwasili mara ya kwanza Stamford Bridge mwaka 2004, wiki chache tu baada ya kuiongoza Porto ya Ureno kunyakua kombe la mabingwa wa Ulaya.

Alishinda kombe kombe la FA na pia Kombe la ligi mara mbili pamoja na ubingwa wa ligi ya England mara mbili.

Ingawa hakuweza kunyakua kombe la klabu bingwa ya Ulaya akiwa na Chelsea.

Uhusiano wake na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich ulizoroteka na akaondoka licha kwamba alibakiza miaka mitatu katika mkataba wake.

Alishinda kombe lake la pili la klabu bingwa ya Ulaya akiwa na Inter Milan ya Italia mnamo mwaka 2010, lakini akaondoka mwaka mmoja baadae kujiunga na Real Madrid ya Uhispania.

Chini ya uongozi wake Real ilimaliza nafasi ya pili katika La Liga katika msimu wake wa kwanza lakini wakashinda ubingwa mwaka mmoja baadae.