Chelsea waibamiza Hull City

Chelsea wapata ushindi wao wa Kwanza chini ya Mourinho.

Magoli 2 yaliyofungwa katika kipindi cha kwanza,moja la Oscar na lingine la Frank Lampard yameiwezesha Chelsea kufunga Hull.

Kabla ya Chelsea kuliona lango,Lampard alikuwa amekosea mkwaju wake wa penalty uliopanguliwa na kipa Allan McGregor,lakini muda mfupi baadae Oscar akanusa nyavu kwa kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na kiungo Kevin de Bruyne.

Lampard aliihakikishia Chelsea kuongoza na kuondoka na ushindi kwa kuingiza bao la pili.

Hull iliyopanda daraja msimu huu, juhudi zake za kujaribu kusawazisha katika kipindi cha pili hazikufua dafu baada ya walinzi wa Chelsea kuwa makini na kudhibiti sawa sawa nafasi zao.

Kwa ushindi huo wa kwanza wa Mourinho tangu aliporudi kuifundisha tena Chelsea,meneja huyo sasa anaweza kuelekeza macho yake na mbinu zake kwa mechi itakayofwatia ,Chelsea itakapoikaribisha Aston Villa jumatano.

Mapema ya hapo,Tottenham walijipatia ushindi wa goli 1 bila kwenye uwanja wa Crystal Palace kupitia mshambuliaji wao mpya Roberto Soldado aliyetikisa nyavu kunako dakika ya 50 kwa njia ya penalty.