Lazio kucheza bila mashabiki

Mchezo wa Lazio
Image caption Lazio katika Serie A

Katika michezo sehemu ya uwanja wa klabu ya Lazio ya Italia imefungwa kwa mechi moja pekee kufuatia mashabiki kuwatusi wachezaji weusi.

Wachezaji watatu wa Juve Mfaransa Paul Pogba, Kwadwo Asamoah na Angelo Ogbonna kutoka Ghana na mchezaji wa Itali mwenye asili ya Nigeria walirushiwa matusi na mashabiki kwenye uwanja wa Stadio Olimpiko mjini Roma.

Hii ina maana kwamba mechi ya kwanza baina ya Lazio na Udinese katika Ligi ya Serie A itafanyika bila mashabiki uwanjani.

Kwingine hata kwa klabu za Arsenal na Fenebahce michuano ya Ligi ya mabingwa Ulaya ni muhimu kutokana na mapato.

Jumatano hii Arsenal iliyozongwa na matatizo inapambana na klabu inayokabiliwa na kesi mahakamani ikitishiwa kuondolewa mashindanoni.

Mawakili wa Fehnebahce wanaanza kusikiliza kesi kwa siku mbili huko Uswizi kuhusu tuhuma za ubadhirifu.

Shirikisho la UEFA liliruhusu klabu hio ishiriki mechi mbili dhidi ya Arsenal ingawa matokeo ya mahakama yanaweza yakaiondolea ushindi hata ikiwa imeshinda mechi ya nyumbani na marudiano mjini London.

Huko India maofisa wa michezo wanatokwa jasho kwa wanariadha wao kukataliwa kushiriki michezo ya Bara Asia kwa sababu ya umri wao uliozidi ule unaoruhusiwa.

Wanariadha 17 wa India wakiwa sehemu ya kikosi cha watu 27 wa India walipatikana kua na zaidi ya miaka 17 inayotakiwa kwenye mashindano haya.