Manchester City yanyolewa na Cardiff

Cardiff yachapa Manchester City
Image caption Cardiff yachapa Manchester City

Hiki ni kichapo cha kwanza kwa Man City kumkaribisha meneja mpya wa Manuel Pellegrini katika ligi ya England.

Mabao mawili yaliyotiwa kimiani na mshambuliaji Fraizer Campbell yameipa ushindi Cardiff City wa magoli 3-2 dhidi ya Manchester City leo kwenye uwanja wa Cardiff.

Edin Dzeko alikuwa ametangulia kuifungia bao City kunako dakika ya 52 lakini likasawazishwa baadae na Aron Gunnarsson.

Alvaro Negredo wa Manchester City ameifungia bao la pili mnamo dakika za majeruhi lakini halikuweza kuepusha kichapo. wakati huo huo Tottenham nao walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Swansea ambalo lilifungwa na mshambuliji Roberto Soldado kwa njia ya penalty katika dakika ya 58.

Leo usiku Manchester United wataikaribisha Chelsea kwenye uwanja wao wa Old Trafford.