Manchester United na Chelsea 0-0

Image caption Jinsi mambo yalivyokuwa uwanjani Old Trafford

Klabu za Chelsea na Manchester United zilimenyana na kutoiana jasho bure katika uwanjani Old Trafford kwani zilitoka sare ya sufuri kwa sufuri.

Matokeo hayo yanamaanisha timu kubwa katika ligi hyo ya Uingereza, wote wamepoteza pointi katika hatuia za awali tangu michuano ianze .

Arsenal walikuwa wakwanza walipozabwa na Aston Villa halafu ikawa zamu ya Manchester City iliyopoteza pointi tatu walipochunwa na Cardiff City siku ya jumapili.

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho aliiambia BBC Sport " Hakuna Upande uliostahili kushinda na kushindwa vile vile, unataka kushinda lakini pande zote zilikua na ulinzi mkali. Na kwa mashabiki najua angalau bao moja lingewafurahisha, iwapo ungekuwa mchuano mzuri''.

Naye meneja wa Manchester United, David Moyes alisema, alivunjika moyo kwa sababu hawakuzoa pointi yoyote, lakini ndivyo ilivyo na hawana budi kujifunza kutokana na hali hiyo.

Chelsea kwa sasa inaongoza ligi kuu kwa pointi saba, ikifuatwa kwa karibu sana na Liverpool na Tottenham, zote zikiwa na pointi sita. Machester United inashikilia nafasi ya nne ikiwa na pointi nne.