Chelsea kuchuana na Bayern Munich

Image caption Kocha wa Chelsea Jose Mourinho

Makocha Jose Mourinho na Pep Guardiolla, kwa mara nyingine tena watafufua uhasama wao leo usiku, wakati mabingwa wa kombe la Uropa Chelsea itakapotoa Udhia na mabingwa wa Ulaya Bayern Munich katika fainali ya kombe la Uefa Super Cup mjini Prague.

Guardiola wa Barcelona na Mourinho wa Real Madrid walikuwa na uhasama mkali kwa misumu miwili, lakini kocha huyu mpya wa Bayern Munich amepuuzilia mbali uhasama kati yao.

Raia huyo wa Uhispania, ambaye alichukua likizo ya mwaka mmoja baada ya kuihama klabu ya Barcelona mwisho wa msimu wa mwaka wa 2011-12, amesema anamuheshimu sana Mourinho, ila nia yake kuu ni kushinda mechi baina yao itakayochezwa leo usiku.

Guardiola alimpiku mpinzani wake katika kinyang'anyiro cha kuwania kombe la ligi ya La Liga mwaka wa 2010-11, lakini kikosi cha Mourinho kiliishinda Barcelona katika kombe la Copa Del Rey msimu huo kabla ya kunyakuwa kombe la ligi kuu msimu uliofuatia.

Image caption Pep Guardiolla

Kikosi cha Mourinho kimewahi kuishinda kikosi cha Barcelona katika mechi tatu pekee kati ya kumi na tano walizocheza.

Kocha huyo kutoka Ureno hajawahi kushinda kombe hilo la Urpo.

Aliongoza FC Porto na Inter Millan kunyakuwa ubingwa wa bara Ulaya na kuviacha vilabu hivyo vikitafuta ubingwa katika kobe hilo.

Mwaka wa 2003, Fc Porto ambao walikuwa mabingwa wa kombe la Uefa walishinda katika fainali hiyo na Valencia.

Wachezaji wapya wa Chelsea Willian na Samuel Eto'o hawajasafiri na timu hiyo hadi Praqu