Nwofor wa Nigeria ajiunga na SC Heerenveen

Image caption Timu ya taifa ya Nigeria

Mshambulizi wa kimataifa wa Nigeria Uche Nwofor amejiunga na klabu ya Uholanzi ya SC Heerenveen, kwa mkpo kutoka kwa klabu ya VVV Venlo iliyoshushwa daraja.

Nwofor mwenye umri wa miaka 21, ambaye alikataa ombi kutoka kwa vilabu vya Urussi na Uturuki, alisaini mkataba wake mpya baada ya kukamilisha uchunguzi wa kimatibabu mapema hii leo.

Aliifungia timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles magoli mawili wakati ilipoilaza Afrika Kusini ka magoli mawili kwa bila wiki mbili zilizopita mjini Durban.

Akiongea na BBC Nwofor alisema, amefurai kusaini mkataba mpya kwa kuwa atapata fursa ya kuimarisha kipaji chake.

''Nitaendelea na masomo yangu ya taalumu ya mchezo wa soka nchini Uholanzi na naamini nimepata klabu inayonifaa'' Alisema mchezaji huyo.

Nwofor ambaye ameweka rekodi ya kuwa mmoja wachezaji wanaofunga magoli, katika kikosi cha wachezaji chipukizi nchini Nigeria, alijiunga na Venlo Septemba mwaka wa 2011 na kufunga magoli kumi na tatu baada ya kucheza mechi hamsini na mbili.

Vilabu bya Arsenal, Tottenham na Newcastle vimehusishwa na mchezaji huyo ambaye amefananishwa na mshambulizi matata wa Aston Villa Christian Benteke.

Mchezaji huyo alikataa kujiunga na klabu ya CSKA Moscow Januari mwaka huu, kwa kitita cha pauni milioni nne na meneja wake Tonny Harris amesema anaimani kuwa mchezaji huyo amechukua uamuzi unaofaa.