Newcastle yapata ushindi wa kwanza

Hatem Ben Alfa
Image caption Hatem Ben Alfa

Goli 1-0 dhidi ya Fulham limetosha kuiwezesha Newcastle kupata alama 3,ukiwa ni ushindi wa kwanza tangu ligi kuu ya England kuanza.

Hatem Ben Alfa Hatem ndiye aliyewezesha Newcastle kumaliza ukame wa mechi 4 bila goli,kufwatia goli alilofunga mnamo dakika za mwisho.

Huo pia umekuwa ushindi wa kwanza wa nyumbani kwa timu hiyo, tangu kuanza kwa michuano ya ligi.

Katika matokeo ya mechi zingine,West Ham wameangushwa nyumbani na Stoke kwa kufungwa bao 1-0 lililofungwa na Jarmaine Pennant kunako dakika ya 82.

Norwich nao wakichezea nyumbani wameifunga Southampton 1-0 huku Cardiff na Everton zikitoka nguvu sawa.

Jumapili hii kunatarajiwa mechi mbili kali ambapo Liverpool itaikaribisha Manchester United na Arsenal kuzipiga na Tottenham.

Chelsea inaongoza ligi ikiwa na alama 7 ikizidi kwa alama moja Manchester City,Liverpool,Tottenham na Stoke.Lakini pia ina mechi moja zaidi kuliko timu zingine.