Bale avunja rekodi ya usajili duniani

Gareth Bale
Image caption Gareth Bale

Real Madrid imevunja rekodi ya dunia ya uhamisho wa wachezaji kwa kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Gareth Bale.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales ametia saini mkataba wa kuichezea Real Madrid wa miaka 6 kwa kununuliwa kitita cha pouni milioni 85,3.

Rekodi iliyokuwepo ilikuwa ya Cristiano Ronaldo aliponunuliwa na Real Madrid toka Manchester United kwa pouni milioni 80 mwaka 2009.

"nilikuwa na furaha ya miaka 6 niliyochezea Spurs,lakini huu ni wakati mwafaka kwangu kusema kwa heri "alisema Bale mwenye umri wa miaka 24.

Bale aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu uliopita katika ligi kuu ya England alijiunga na Tottenham kutoka Southampton kwa pouni milioni 10 mwaka 2007 na alifunga magoli 26 msimu uliopita.