Golikipa mchezaji bora Ulaya

Golikipa wa Timu ya Taifa ya wanawake Ujerumani Nadine Angerer ameshinda tuzo yua mwanamke bora kati ya wacheza soka wanawake barani Ulaya.

Image caption Nadine Angerer

Angerer, atakayeanza kucheza soka yake nchini Marekani mwaka ujao, aliwashinda wachezaji kutoka timu yake ya Ujerumani Lena Goessling na mchezaji wa Sweden Lotta Schelin ambaye ni mshambuliaji.

Itakumbukwa kuwa Angerer aliweza kuzuia mikwaju ya peneti mara mbili katika fainali ya Ulaya mwaka 2013 mwezi julai, na hivyo kuisaidia Ujerumani kuishinda Norway 1-0.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 atacheza soka yake huko Australia akichezea klabu ya Brisbane Roar kabla ya kujiunga na klabu inayoshiriki Ligi ya wanawake ya soka.

Angerer anasema kua, bado hayo hayajathibitishwa lakini kwa vyovyote mipango hiyo itaanza mwaka 2014.

Pia alishinda tuzo ya UEFA kutokana na kura zilizopigwa na wandishi wa habari za michezo zilizopendekezwa na wakufunzi wa timu za wanawake zinazoshiriki Ligi ya mabingwa.