Real Madrid yatangaza faida

Nembo ya Real Madrid
Image caption Nembo ya Real Madrid

Siku chache tu baada ya kutumia kitita kikubwa kumsajili Gareth Bale kutoka klabu ya Tottenham hotspurs ya England Real Madrid imetangaza kupanda kwa faida katika mapato yake na punguzo la asili mia 27.4 ya deni lake katika kipindi cha msimu wa mwaka 2012/13. Magwiji hao wa soka ya Uhispania wamejionea mapato yao yakipanda hadi Euro milioni 520.9

Mapato hayo hayahusishi udhamini mkubwa wa Fly Emirates wa shati za klabu unaokadiriwa kua euro milioni 29 kwa kila mwaka kuanzia msimu huu.

Pamoja na usajili wa Bale, Real ilitumia euro milioni 70 kwa kuwapata Isco na Asier Illarramendi.

Vilevile klabu hio ilirejesha takriban euro milioni 100 katika kuwauza wachezaji wake Mesut Ozil aliyejiunga na Arsenal kunako siku ya mwisho wa usajili na Gonzalo Higuain, Raul Albiol na Jose Maria Callejon waliojiunga na Napoli mwezi julai.

Uwamuzi wa Kaka kuondoka Real Madrid na kurudi AC Milan pia kulipunguza kiwango cha mishahara ya klabu hiyo kwa mshahara wake wa euro milioni 10 kwa mwaka wake wa mwisho lau kama angehitimisha mkataba wake.