Mayweather adhihirisha ubingwa wake

Image caption Mayweather ni bingwa wa dunia

Floyd Mayweather ameboresha umaarufu wake kama bingwa wa masumbwi baada ya kumshinda Saul Alvarez mjini Las Vegas.

Ushindi wa Mayweather mwenye umri wa miaka 36, umempa taji la WBC na WBA uzani wa kati. Pia ameshinda katika michuano yote 45 aliyopigana kama mwanamasumbwi wa kulipwa.

Majaji walimpa pointi, 114-114, 116-112, 117-111.

Mayweather hakuwahi kutishika na hata kumfanya mshindani wake kufanana tu na mtu wa kawaida.

Aidha bingwa huyu wa dunia atapokea kitita cha dola milioni 45 kwa juhudi zake, na kumfanya kuwa mwanamasumbwi aliyelipwa pesa nyingi zaidi duniani kwa mchuano mmoja.

Huku watazamaji wakiwa wamenunua tiketi ya kujionea mechi kwa dola 30,000, kila tiketi, wengi walitarajia kuwa Avarez mwenye umri wa miaka 23, angetifua kivumbi na angalau kumweka tumbo joto Mayweather, lakini wapi.