United yachapwa na West Brom

Image caption Kocha David Moyes

Umekuwa usiku mwingine mbaya sana kwa meneja David Moyes,timu yake ya Manchester United ilipochapwa na West Brom 2-1 Old Trafford.

Goli la mshambuliaji Saido Berahino limeiwezesha West Brom kupata ushindi wake wa kwanza kwenye uwanja wa United tangu mwaka 1978.

Morgan Amalfitano alikuwa ametangulia kwa kufunga goli la kwanza muda mfupi baada ya kuanza kwa kipindi cha pili.

Goli hilo lilikombolewa na Wayne Rooney dakika chache baadae lakini halikuzuia kichapo. Kushindwa kwa United kumethibitisha mwanzo wake mbaya wa ligi kuwahi kutokea tangu msimu wa ligi wa 1989-90. Kichapo hicho kinafwatia kingine cha mabao 4-1 walichopata dhidi ya mahasimu wao Manchester City wiki iliyopita.