Norwich yaibwaga Stoke

Aaron Ramsey
Image caption Aaron Ramsey

Klabu ya Norwich imejipatia ushindi wake wa pili wa Ligi kuu ya England kupitia bao la Jonny Howson katika kipindi cha kwanza kuibwaga Stoke.

Howson alizitikisa nyavu za Stoke kutoka umbali wa yadi 25 kwa mkwaju wa chini katika mechi iliyokua na upungufu wa fursa chache.

Hata hivyo nyota ya Norwich ilionekana mapema baada ya mkwaju wa mshambuliaji Ryan Bennett kugonga besera na mpira uliporudi uwanjani golikipa Asmir Begovic akazuia juhudi za washambuliaji wa Norwich.

Kwa kipindi kizima cha mchuano Stoke iliweza kujaribu mara moja kufanya shambulizi ambapo Steven Nzonzi alilazimisha golikipa wa Norwich John Ruddy kuinama ili kupooza mkwaju wa kutoka masafa marefu.

Arsenal na Swansea

Wakati huo huo mcheza kiungo wa Wales na Arsenal Aaron Ramsey anasema alifurahia kufunga katika ushindi wa Arsenal 2-1 dhidi ya klabu Swansea kwenye uwanja wa Liberty hapo jana.

Mchezaji huyo aliyeichezea watani wa Swansea, Cardiff City alizomewa kupitia kiupindi chote cha mchuano na mashabiki wa Swansea.

Bao la Ramsey lilipatikana katika dakika ya 62 kuipa klabu yake ya Arsenal mabao mawili kuthibitisha mwendo wao wa kushinda.

Ushindi wa Arsenal umeizidishia klabu hiyo rekodi ya kushinda ugenini kutimiza mechi 12 ikiwa ni sawa na rekodi yao ya mechi nane katika Ligi ya Premier iliyowekwa katika msimu wa mwaka 2001-02.

Katika ushindi wa jumamosi, Ramsey, aliyejiunga na Arsenal mwaka 2008 akiwa kija na mwenye umri wa miaka 17 na baada ya hapo kukumbwa na jeraha lililomueka nje ya mchezo ka kipindi kirefu na baada ya hapo kushindwa kufikia viwango na kukemewa na mashabiki hapo jana alikua chachu ya ushindi dhidi ya Swansea.