Liverpool yapanda kileleni

Suarez
Image caption Luis Suarez

Mshambuliaji Luis Suarez amefunga bao katika mechi yake ya kwanza kwenye uwanja wa Anfield tangu mwezi April kwa ushirikiano na mshambuliaji mwenzake Daniel Sturridge kuiwezesha Liverpool kuibwaga Crystal Palace.

Raia huyo wa Uruguayan, aliyetumikia kifungo cha mechi 10 kwa kumngata beki wa Chelsea alifunga bao safi katika kipindi cha kwanza akiwa anagaragara chini.

Kisha Sturridge akaziona nyavu baada ya kuwatatiza mabeki wa Palaca na baadaye nahodha Steven Gerard akamilizia kwa mkwaju wa peneti.

Ushindi huo unaiweka Liverpool kileleni mwa Ligi kuu ya England kwa pointi 16, moja mbele ya Arsenal na City katika nafasi ya tatu.

Newcastle na Cardif Mfaransa Loic Remy alifunga mara mbili kuiwezesha Newcastle kustahamili mikiki mikiki ya Cardif iliyobadilika katika kipindi cha pili ikitafuta ushindi dhidi ya wageni.

Fulham na Stoke

Mashabiki wa Fulham walimzomea kocha wao kwa matokeo ya awali na hali mbovu inayoonyeshwa na klabu yao.

Lakini kocha Martin Jol alimleta mshambuliaji Darren Bent kutoka meza ya wachezaji wa ziada kuipatia Fulham bao pekee la ushindi na kumpunguzia dhiki kocha wake.

Kwingine Hull City iliendelea kudhibiti rekodi yake ya kutopoteza kwenye uwanja wa nyumbani na kuikwamisha Aston Villa ikiridhika kwa matokeo ya 0 -0.