Man Utd yakosa mwelekeo

Wachezaji wa Man United
Image caption Wachezaji wa Man United

kwa mara nyingine tena Manchester United imeandikisha matokeo mabaya kwa kutoka sare nyumbani.

Goli lililofngwa na nahodha Adam Lallana dakika moja kabla ya mechi kumalizika,limeiwezesha Southampton kuondoka na alama 1 kwenye uwanja wa Old Trafford.

Manchester United imepata goli la kuongoza katika dakika ya 25 ya mchezo.

Matokeo hayo ya goli 1-1 ni ya kuvunja moyo kwa mashabiki wa Manchester United ambayo imekwisha funga mechi 2 tu miongoni mwa mechi 7 na sasa iko nyuma ya viongozi wa ligi Arsenal kwa alama 8.

Katika matokeo mengine ya mechi zilizochezwa,Chelsea waliinyuka Cardiff magoli 4-1;Everton ikailaza Hull 2-1;Swansea iliichapa Sunderland 4-0 Stoke wakatoka sare bila kufungana na West Brom.