Sir Alex Ferguson awapa moyo Man U

Image caption Ferguson alistaafu baada ya kuiongoza klabu kwa miaka 27

Aliyekuwa kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema kuwa wachezaji wa Man U wanaweza kubadili mwanzo wao mbaya kwenye ligi ya Premier, licha ya kuwa pointi nane nyuma ya timu inayoongoza ligi hiyo kwa sasa Arsenal.

Ushindi mara mbili wa timu hiyo katika mechi mbili zilizopita , ina maana kuwa upande wa David Moyes wameweza kujikomboa kutokana na matokeo mabaya zaidi ya Man U katika mwanzo wa ligi hiyo, kuwahi kushuhudiwa katika miaka 24 ya klabu hiyo.

Ferguson, mwenye umri wa miaka 71, alisema sio mara ya kwanza kwa klabu hiyo kuwa na mwanzo mbaya wa msimu. Imetokea mara nyingi.

"Man U ndio klabu pekee kuwahi kutoka nyuma kwa pointi na hatimaye kushinda ligi,'' alisema Ferguson

Ferguson, aliyesalia kuwa mmoja wa wakurugenzi wa klabu hiyo , alistaafu kutoka katika wadhifa wa meneja mkuu wa klabu mwishoni mwa msimu baada ya kushinda mataji 38 katika usimamizi wake wa miaka 27.

Naye menaja mpya Moyes anakumwba na wakati mgumu upande wa mashabiki baada ya kuanza vibaya msimu.