Kocha wa Wales kujadili Mkataba wake

Image caption Kocha wa Wales Chris Coleman

Kocha wa timu ya soka ya Wales Chris Coleman atakutana na maafisa wa chama cha soka cha Wales hii leo kujadili kuhusu mkataba mpya.

Coleman ambaye mkataba wake unamalizika baada ya mchezo kati ya Wales na Finland tarehe 16 mwezi Novemba, ameelezwa kupigiwa pande kuziba nafasi iliyo wazi kwenye timu ya Crystal Palace

Tetesi kuhusu mustakabali wa Coleman ziliongezeka baada ya kuahirishwa kwa mkutano wa waandishi wa habari hii leo uliokuwa umelenga kutaja kikosi kitakachovaana na Finland, huku maafisa wa Wales wakisema kuwa wamejadiliana na Chris na kuamua kuwa watataja kikosi hicho kwa njia ya barua pepe.

Msemaji wa chama cha mpira cha Wales amesema kuwa wanaona kuwa zoezi la kuita mkutano wa waandishi wa habari hautakuwa na maana kwa kuwa maswali yatajielekeza kuhusu mkataba wa Chris na mipango ya kuhamia Crystal Palace.

Klabu ya crystal Palace ambayo Coleman amekuwa akiichezea kwa miaka minne imekuwa ikitafuta Kocha mpya baada ya kuondoka kwa Ian Holloway kuondoka mwezi uliopita.

Mkataba mpya wa Coleman utakuwa kwenye ajenda katika mkutano kati yake na maafisa wa Chama cha soka cha Wales zikiwa zimebaki siku nane pakee kabla ya mkataba wake wa sasa kumalizika.