Jonarthan Pitroipa

Jonarthan Pitroipa

Matunda ya mwanasoka Jonarthan Pitroipa kuibuka kuwa mmoja wa watakao wania tuzo ya BBC yalionekana hasa baada ya kuanza kwa michuano ya kombe la mataifa barani Afrika, ambapo Burkina Faso ilipangwa katika kundi gumu likiwa na Timu ya Zambia na Nigeria.

Si tu walifanikiwa kuing’oa Chipolopolo, mabingwa watetezi, pia waliongoza kundi hilo wakiwa mbele ya Nigeria.

Super Eagles ilifanya jitihada za kuishinda Burkinabe katika mchuano wa fainali, mwishowe hakuna mchezaji mwingine yeyote wa Nigeria isipokuwa Pitroipa wa Burkinafaso aliyechaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye michuano hiyo.

Winga huyo kutoka klabu ya Rennes amekuwa chachu ya kufanya vizuri, akisawazisha bao dakika za mwisho katika mpambano wa ufunguzi na mchuano uliofuata akifunga bao moja na kutengeneza mawili wakati timu yake ilipokuwa ikicheza huku wakiwa kumi na kuibuka washindi wa mabao 4-0

Huo ulikuwa ushindi wa kwanza wa Stallion katika michuano ya kombe la mataifa barani Afrika tangu iliposhika nafasi ya nne mwaka 1998 timu hiyo ilipokuwa mwenyeji wa mashindano ambapo Pitroipa aliisaidia timu yake kuingia kwenye raundi ya nusu fainali alipoifungia timu yake bao 1-0 wakati wa muda wa nyongeza walipochuana na Togo.

Pitroipa aliondolewa kimakosa kwa adhabu ya kadi nyekundu kwenye hatua ya nusu fainali timu yake ilipocheza na Ghana , Nyota huyo wa zamani wa Hamburg hatimae alicheza mchezo wa fainali baada ya adhabu ya kadi nyekundu kutenguliwa, hata hivyo Burkinafaso ilipoteza mchezo huo kwa kufungwa goli 1-0.

Wadadisi wana tathmini gani kumhusu Jonarthan?

Hakuna mchezaji yeyote wa Burkinafaso aliyefikia hatua ya kushinda tuzo ya BBC ya mchezaji bora wa Afrika wa mpira wa miguu wa mwaka , lakini Jonathan Pitroipa anastahili.

Ni mmoja kati ya wachezaji mahiri wenye kipaji, Winga huyu akifurahisha uwanjani, akiupamba mchezo na namna anavyo tumia ufundi wake katika kumiliki mpira na kasi ya kupenya adui.

Nyota ya Pitroipa ilianza kung’aa katika kombe la mataifa ya Afrika, na zaidi fainali za mwaka huu zilizomfanya kuwa Mchezaji wa Burkinafaso wa kwanza kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano hayo.

Ni muhimu kulitilia hili maanani kwa kuwa Timu ya Burkinafaso ilisafiri mpaka Afrika kusini huku wakiwa hawana rekodi yeyote ya ushindi kwa mashindano 21 ya mataifa ya Afrika katika nchi ya kigeni.

Hii ilibadilisha historia ya ushindi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Ethiopia, huku Winger huyo wa Rennes amefanikisha katika kufungwa kwa magoli matatu kati ya manne, kabla ya kuishinda Togo kwenye mchezo wa robo fainali, Burkinabe iliingia nusu fainali kwa mara ya kwanza mwaka 1998, wakati huo Pitroipa akishuhudia michuano hiyo akiwa na umri wa miaka 11.