Rice agundulika kuwa na saratani

Image caption Kocha msaidizi wa zamani wa Asenal, Pat Rice

Mchezaji wa zamani wa timu ya Ireland kaskazini na mlinzi wa zamani wa Arsenal Pat Rice amefikishwa hospitalini baada ya kugundulika kuwa na ugonjwa wa Saratani.

Rice mwenye umri wa miaka 64 aliichezea mara 528 timu ya washika Bunduki wa London pia aliwahi kuwa Kocha msaidizi akimsaidia Arsene Wenger kwa kipindi cha miaka 16 kabla ya kustaafu mwaka 2012.

Taarifa ya klabu ya Arsenal imethibitisha kuwa Pat yu hospitali akipata matibabu na kumtumia salamu za pole na kumtakia heri apone haraka.

Rice aliichezea Gunners kwa kipindi cha zaidi ya misimu 14 baada ya kujiunga na timu ya vijana, ambapo timu yake ilichukua ubingwa wa Kombe la Ligi na FA mara mbili ,mwaka 1971, pia alikuwa nahodha wa Timu hiyo ambayo ilipata mafanikio makubwa kwenye michuano ya FA mwaka 1979.

Wenger amesifu jitihada na kazi ya Rice ambaye alikua akifanya nae kazi mpaka alipostaafu mwaka 2012.