Everton yailaza Man U 1-0

Image caption Everton walishinda Man U kwa bao moja bila

Klabu ya Everton iliingiza bao la dakika za mwisho na kujipatia ushindi wake wa kwanza wa bao moja bila dhidi ya Manchester United katika miaka 21 ya klabu hiyo.

Ushindi huu dhidi ya Man umemuongeza masaibu tele meneja wa klabu hiyo David Moyes ambaye klabu yake inaonekana kuendelea kushuka ngazi .

Mlinzi wa Everton Bryan Oviedo, aliingiza bao la dakika za mwisho kuhakikisha meneja wao Roberto Martinez alipata ushindi wa mara ya kwanza na kumuondolea bahati yoyote Moyes ya Man U kushinda.

Moyes alizomewa muda wote wa mechi na mashabiki waliokasirishwa na alivyoondoka.

Oviedo alichukua nafasi ya Baines aliyekuwa na jeraha.

Moyes na wachezaji wake ina maana hawakuwa na bahati kamwe, hasa kwa kua Wayne Rooney na Danny Welbeck walikuwa wachezaji wa akiba lakini ushindi ulikuwa kitu muhimu sana kwa Everton na kocha wao, Martinez.

Martinez alipongezwa mno na mashabiki wa klabu, mechi ilipokamilika huku Everton wakishikilia nafasi ya tano kwenye ligi hiyo. Man U wanashikilia nafasi ya tisa wakiwa na pointi kumi na mbili nyuma ya Arsenal.

Man U pia walikosa huduma za mchezaji wao Robin van Persie.