Man U kipigo mfululizo

Image caption Wadadisi wanasema ikiwa Man U itaendelea kushindwa huenda isiwe katika nafasi za kwanza nne

Manchester United Jumamosi lipata kipigo chake cha pili nyumbani katika muda wa siku nne baada ya kulazwa bao moja bila na New Castle.

Mchezaji wa New Castle Yohan Cabaye ndiye aliipatia kilio Man U huku kwao ikiwa kicheko baada ya kushinda Manchester United kwa mara ya kwanza nyumbani Old Trafford tangu mwaka 1972.

Man U walikuwa na wakati mgumu kuvunja ari ya Magpies na kukosa nafasi kadhaa za mabao mfano Patrice Evra alipogonga lango huku mpira ukirudi na kumgonga mkono Vurnon Anita.

Mpira wa kichwa wa Robin van Persie haukuzaa matunda kwa Manchester United,lakini Newcastle waliishia na kicheko baada ya kupata ushindi wao wa kihistoria dhidi ya Man U.

Bila shaka hii inazua wasiwasi mkubwa kwa David Moyes kwani Man U wanaendelea tu kudidimia kwa mabao.

Man u wameshuka ngazi hasa baada ya kupata kipigo mara mbili mfululizo tena nyumbani Old Trafford ikiwa ni mara ya kwanza kwa hali hii kushuhUdiwa kwa United.

Mnamo Jumatano walilazwa na Everton huku wakiwa nyuma ya Arsenal kwa pointi 12 wakikabiliwa na tisho la kutokuwa katika msitari wa mbele kuwania kombe la ligi ya Premier.

Ikiwa wataendelea kushindwa hivi Man U hata huenda wasiwe katika nafasi za kwanza nne.