Arsenal wabwagwa na Man City 6-3

Image caption Man City wamekuwa wakicheza vyema sana wadadisi wanasema ikiwa wataendelea hivyo huenda wakashinda ligi

Manchester City, wametoa ujumbe mkali kwa mahasimu wao kwenye ligi ya Premier Arsenal baada ya kuwacharaza mabao sita kwa matatu.

Upande wa Manuel Pellegrini uliwacharaza Arsenal na kuziba pengo la pointi tatu.

Arsenal walilalamika wakitaka kupewa penalty moja ingawa kwa kweli Man City walikuwa wamejiandaa vilivyo dhidi ya Arsenal, huu ulikuwa kama upepo kwao.

Man City sasa wameingiza mabao 35 nyumbani katika mechi 58 katika uwanja wa Etihad.

Msimu huu City hawacharazi tu timu nyumbani bali wanang’oa pembe zao na ikiwa wanaweza kuonyesha mchezo kama huu hata wanapocheza ugenini bila shaka watakuwa katika msitari wa mbele kushinda kombe la ligi ya Premier.

Bao la Sergio Aguero lilifuatiwa na bao laTheo Walcott aliyecheka na wavu, lakini Alvaro Negredo akaiwezesha City kusalia mbele kabla ya kipindi cha kwanza cha mchezo.

Fernandinho aliiweka City mbele wakati wote ingawa Walcot aliingiza bao lengine la pili kabla ya City kuanza kushambulia Arsenal kutoka pande zote hasa baada ya David Silva Fernandinho tena kuingiza bao lengine kabla ya Per Mertesacker kuyanfa mabao 5-3 kabla ya mechi kumalizika.

City walifikisha mabao yao kuwa sita kufuatia penalti ya Yaya Toure kabla ya mechi kumalizika.