Timu16 bora zitakazokutana Uefa

Image caption Rais wa UEFA Michel Platini

Droo ya timu zitakazokutana katika hatua ya 16 bora ligi ya mabingwa ulaya imefanyika ambapo Manchester City imepangwa kumenyana na Barcelona huku Arsenal wakipangwa kukutana na Bayern Munich.

Kwa upande wake Chelsea wataumana na Galatasaray huku Manchester United wakikutana na Olympiakos ya Ugiriki.

Droo hiyo pia imezikutanisha AC Milan na Atletico Madrid huku Bayern Leverkusen ikipangwa kukutana na Paris St- Germain ya Ufaransa. Schalke itakutana na Real Madrid na Zenit Petersburg wakiorodheshwa kumenyana na Borussia Dortmund.

Droo kamili hii hapa nchini

Manchester City v Barcelona Olympiakos v Manchester United AC Milan v Atletico Madrid Bayer Leverkusen v Paris St-Germain Galatasaray v Chelsea Schalke v Real Madrid Zenit St Petersburg v Dortmund Arsenal v Bayern Munich

Mechi hizo zitachezwa kama ifuatavyo:

Tarehe 18/19/25/26 February (mzunguko wa kwanza ) Tarehe 11/12/18/19 March (mzunguko wa pili) Robo Fainali : 1/2 April and 8/9 April Nusu Fainali: 22/23 April and 29/30 April Fainali: 24 May