Adebayor adai kutoheshimwa na Tottenham

Image caption Emmanuel Adebayor

Mshambuliaji wa Tottenham, Emmanuel Adebayor, amesema kuwa wasimamizi wa klabu hiyo hawamuheshimu.

Adebayor, alifunga magoli mawili katika mechi yake ya kwanza msimu huu pale Tottenham, ilipoilaza Southampton kwa magoli matatu kwa mawili siku ya jumapili.

Lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka ishirini na tisa, hakujumuishwa kwenye picha rasmi ya klabu hiyo na alikuwa akifanya mazoezi pekee waki Andre Villas-Boas alikuwa kocha.

But the 29-year-old forward was not included on the club's official

''Ilikuwa ngumu sana, wakati nikija kufanya mazoezi na kuona picha ya klabu yangu ambayo sijajumuishwa, hiyo inamaanisha kuwa wao hawaniheshimu'' Alisema Adebayor.

Adebayor, aliichezea Tottenham kwa mkopo kutoka klabu ya Manchester City mwaka wa 2011-12 na alifunga magoli kumi na saba baada ya kuichezea mechi thelathini na tatu, kabla ya kujiunga na Spurs kwa mkataba wa kudumu agosti mwaka wa 2012 kwa kitita cha pauni milioni tano.

Lakini katika msimu wa mwaka wa 2012-13, Adebayor alifunga magoli matano baada ya kucheza mechi thelathini na sita na msimu huu alicheza dakika arubaini na tano pekee wakati wa Villas-Boas alikuwa kocha.

Septemba mwaka huu, ilitangazwa kuwa Adebayor huenda akakihama klabu hiyo Januari mwaka ujao.

Lakini licha ya vilabu vingi kuonyesha nia ya kutaka kumsajili, mchezaji huyo hajaonesha dalili ya kutaka kuondoka.

Baada ya Villas-Boas, kufutwa kazi wiki iliyopita na Tim Sherwood kuchukua mahala pake, kocha huyo mpya alimjumuisha Adebayor katika kikosi cha wachezaji wake kumi na mmoja wa kwanza.

Katika mechi yao dhidi ya West Ham siku ya Jumatano Adebayor alifunga goli moja na mawili wakati wa mechi yao dhidi ya Southampton siku ya Jumapili.