Man U, Man City zashinda kwa tabu

Image caption Robin van Persie wa Manchester United

Timu zinazotoka jiji moja la Manchester, Manchester City na Manchester United jumamosi zilishinda mechi zao kwa ushindi mwembamba.

Wakati Manchester City wakiwa nyumbani wakiifunga Crystal Palace goli 1 - 0, Manchester United wao waliiadhibu Norwich City kwa goli 1- 0.

Goli la Manchester City lilifungwa na Edin Dzeko katika dakika ya 66 baada ya kupata basi kutoka kwa Navas kutoka upande wa kulia kisanduku cha 18, na kumwachia mfungaji kuukwamisha mpira huo kuwafurahisha mashabiki waliojaa tele kwenye uwanja wa Etihad.

Man U walipata goli lao katika dakika ya 57 kupitia kwa mshambuliaji wao Danny Welbeck aliyeingia kuchukua nafasi ya mkongwe Ryan Giggs.

Line up ya Norwich vs Manchester United:

Norwich: Ruddy, Martin, Ryan Bennett, Bassong, Olsson, Johnson, Fer, Snodgrass, Hoolahan, Redmond, Hooper. Subs: Whittaker, van Wolfswinkel, Bunn, Elmander, Garrido, Becchio, Murphy.

Man Utd: De Gea, Smalling, Evans, Vidic, Evra, Young, Cleverley, Carrick, Giggs, Kagawa, Hernandez. Subs: Anderson, Lindegaard, Welbeck, Fabio Da Silva, Fletcher, Zaha, Januzaj.

Line ups ya Man City v Crystal Palace:

Man City: Hart, Boyata, Kompany, Nastasic, Clichy, Fernandinho, Javi Garcia, Jesus Navas, Silva, Milner, Dzeko. Subs: Lescott, Nasri, Negredo, Kolarov, Rodwell, Pantilimon, Toure.

Crystal Palace: Speroni, Delaney, Mariappa, Gabbidon, Parr, Puncheon, Ward, Bannan, Jedinak, Bolasie, Jerome. Subs: Campana, Phillips, Gayle, Jonathan Williams, Moxey, Chamakh, Price.