Mourinho amtetea refa Artkinson

Image caption Oscar mchezaji wa Chelsea

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema kuwa nyota wake Oscar, amekiri kujiangusha ili kupewa penalti wakati wa mechi yao dhidi ya Southampton, ambayo Chelsea ilishinda kwa magoli matatu kwa bila.

Wakati wa mechi hiyo, Oscar, alijaribu kujiangusha kwenye eneo la hatari kwa lengo la kumshinikiza refa wa mechi hiyo kutoa adhabu ya penalti na pia kuumpa kipa wa Southampton kadi nyekundu.

Hata hivyo refa wa mechi hiyo alipuuza tukio hilo ambalo lilitokea dakika chache tu baada ya Oscar kuingia uwanjani kuchukua mahalam pa Juan Mata na badala yake kuumpam Oscar kadi ya njano.

Mourinho amesema refa huyo Martin Artkinson alichukua uamuzi bora.

Wakati huo huo Mourinho hajamshutumu Mata ambaye hakufurahishwa na uamuzi wake wa kumuondoa uwanjani.

Image caption Jose Mourinho

Uasi huo sasa unaashirikia kuwa mcheza kiungo huyo kutoka Uhispania huenda akakihama Chelsea baadaye mwezi huu, baada ya vilabu kadhaa vinavyoshiriki katika ligi ya La Liga kuonyesha nia ya kutaka kumsajili.

Kocha huyo amesema hana nia yoyote ya kuchochea uhamisho wowote kwa kuwa anataka Mata kusalia na Chelsea, ila amekiri kuwa yuko tayari kusikilizam mchezaji yeyote.

Southampton imeshinda mechi moja peke kati ya mechi tisa zilizopita licha ya kuwa bado wangali katika nafasi za kwanza kumi bora.

Kocha wa Southampton Mauricio Pochettino amesema jukumu lake kuu mwezi huu ni kuhakikisha kuwa wachezaji wake wazuri wote wanasalia na klabu hiyo.

Adam Lallana amejumuishwa kwenye kikosi cha Uingereza nate Luke Shaw amehusishwa na vilabu vya Chelsea na Manchester United.