Liverpool yaiadhibu Stoke 5 - 3

Image caption Liverpool ni ye nne kwenye orodha ya Premier League

Liverpool jumamosi iliwanyoa Stoke City kwa jumla ya magoli 5 -3 katika mchezo wa ligi kuuu ya England na kuifanya ipunguze pointi dhidi timu iliyopo juu ya msimamo wa ligi hiyo na sasa ina pointi tano nyuma ya Manchester City wanaongoza ligi hiyo.

Hiyo ni kabla ya mechi ya Arsenal waliotarajiwa kumenyama na Aston Villa.

Luis Suarez alifunga magoli mawili katika mechi hiyo wakati naye Steven Gerrald akipachika goli huku Daniel Sturridge akiwa miongoni mwa waliofunga magoli.

Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers amefurahia ushindi huo wakati kocha wa Stoke Mark Hughes alihuzunishwa na matokeo hayo.

Kurejea kwa Daniel Sturridge ambaye alikuwa akisumbuliwa na kifundo cha mguu ambaye aliingia kipindi cha pili kuliongeza chachu kubwa katika safu ya ushambuliaji.