Nasri ajeruhiwa vibaya

Image caption Kocha wa City alimlaumu refa kwa kukosa kumuadhibu Yanga-Mbiwa aliyemjeruhi Nasri

Mchezaji wa kiungo cha kati, wa Manchester City Samir Nasri, atafanyiwa uchunguzi zaidi wa jereha la goti alilopata wakati wa mechi ya klabu hiyo dhidi ya Newcastle.

Nasri aliondoshwa uwanjani baada ya kufanyiwa masihara na Mapou Yanga wakati wa mechi yao ambapo walishinda mabao mawili kwa nunge

Kocha wa City Manuel Pellegrini alighadhabishwa mno na tukio hilo na kusema kuwa mtu aliyepaswa kuadhibiwa ni Yanga-Mbiwa.

"Nasri amepata jeraha baya sana. Ilipaswa kuwa kadi nyekundu kwa Yanga,'' alisema Pellegrini

"alijeruhiwa vibaya lakini tutajua hali yake Jumatatu,'' aliongeza kusema kocha huyo.

Meneja wa Newcastle hata hivyo alimtetea Yanga-Mbiwa.

"haikuwa nia yake kumjeruhi Nasri," alsema kocha Pardew. " hiyo sio kawaida yake na natumai kuwa Nasri yuko salama.''

Nasri ambaye huchezea timu ya kitaifa ya Ufaransa, aliondoka uwanjani dakika ya 79 na kupokea matibabu kwa dakika chache, kabla ya kuondoka akiwa analia kwa uchungu

Yanga-Mbiwa hata hivyo alipata onyo la refa.

Kocha Pellegrini pia alithibitisha kuwa Edin Dzeko, aliyeingiza bao lililowapa ushindi City na kuwaweka katika nafasi ya kwanza katika ligi ya premier, alipata jeraha la mguu