Uganda yaanza vizuri CHAN

Image caption Magoli ya Uganda yalifungwa na Mshambuliaji Junior Yunus Sentamu

Timu ya Taifa ya Uganda The Cranes ambayo ni miongoni mwa timu kutoka Afrika Mashariki Jumapili iliwafurahisha mashabiki wake baada ya kuishikisha adabu Burkina Faso kwa jumla ya magoli 2 -1 katika mechi ya kundi B ya michuano Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN.

Magoli ya Uganda yalifungwa na Mshambuliaji Junior Yunus Sentamu ambaye alikuwa ndiye mchezaji bora katika mechi hiyo.

Mechi hiyo iliamsha furaha ya mashabiki wa Uganda ambao walishangilia hata nje ya uwanja huku wakiisifu timu yao kwamba imeonyesha kiwango cha hali ya juu na inaweza kufika mbali katika mashindano hayo.

Mechi nyingine ya kundi B Zimbabwe ilitoka sare ya kutokufungana na Moroco. Jumanne Ghana walitarajiwa kumenyana na Congo Braziville huku Libya nao wakitarajiwa kupepetena vikali na Ethiopia katika mechi nyingine za kundi C.